Rais wa Mauritania Mohamed Ghazouani ashinda muhula wa pili

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Mauritania Mohamed ould Ghazouani amechaguliwa kwa muhula wa pili, baada ya kuibuka mshindi wa uchaguzi mkuu wa Jumamosi iliyopita.

Tume ya uchaguzi nchini humo imetengaza kuwa Ghazouani amepata asilimia 56, ya kura zote akiwashinda waaniaji wengine sita waliowania kiti hicho.

Mwanaharakati anayepinga utumwa Biram Dah Abeid alichukukua nafasi ya pili kwa asilimia 22, huku Hamadi Sidi el-Mokhtar wa chama cha Islamist Tewassoul akipata asilimia 13 katika nafasi ya tatu.

Rais huyo anayehudumu kwa muhula wa pili wa miaka mitano ndiye wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia, kufuatia utawala wa miongo kadhaa ya machafuko ya kisiasa na mapinduzi ya serikali.

Hata hivyo ni asilimia 55 pekee ya wapiga kura waliosajiliwa walioshiriki zoezi hilo.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *