Rais wa CAF Motsepe,yuko Nairobi,atarajiwa kukagua viwanja leo

Kenya inashirikiana na majirani Tanzania na Uganda kuandaa  patashika hiyo ya 36, kati ya Juni na Julai mwaka uja.

Dismas Otuke
1 Min Read
Patrice Motsepe

Rais wa Shirikisho la kandanda barani Afrika Patrice Motsepe,anatarajiwa kufanya ukaguzi wa viwanja vya Kenya leo kwa maandalizi ya kipute cha mataifa ya Afrika AFCON mwaka ujao.

Motsepe alitua Nairobi Alhamisi usiku akitokea Dar es Salaam,Tanzania ambapo pia aliakagua uwanja wa kitaifa wa Benjamin Mkappa.

Ziara ya Motsepe ni ya hivi punde huku ikisalia miezi tisa pekee kabla ya kuanza kwa kindumbwendumbwe  hicho kinachoandaliwa Afrika mashariki kwa mara ya kwanza.

Kenya inashirikiana na majirani Tanzania na Uganda kuandaa  patashika hiyo ya 36, kati ya Juni na Julai mwaka uja.

Uwanja wa Kasarani unakarabatiwa tayari kwa kipute hicho huku ule wa Talanta ukiwa takriban asilimia 90 kukamilika.

Share This Article