Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika ,Dkt Patrice Motsepe anatarajiwa kuwasili nchini leo alasiri kwa ziara ya siku mbili.
Dkt Motsepe anatarajiwa kuwasili katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta saa tisa unusu alasiri.
Mida ya saa kumi kasorobo Dkt Motsepe atakagua ukarabati unaoendelea wa uwanja wa kimataifa wa Kasarani na baadaye saa kumi unusu azuru ujenzi wa uga wa Talanta City .
Viwanja hivyo viwili vitatumika kwa maandalizi ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2027 pamoja na majirani Tanzania na Uganda.
Hapo kesho Dkt Motsepe ataongoza mkuntano wa baraza kuu la CAF jijini Nairobi.
Ni mara ya kwanza kwa Motsepe kuzuru Kenya tangu ashike hatamu za uongozi wa CAF.