Rais wa Angola afanya ziara rasmi nchini Kenya

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais wa Angola João Lourenço na mke wake Ana Dias Lourenço, wazuru Kenya.

Rais wa Angola João Lourenço, anatarajiwa kufanya ziara rasmi ya siku mbili hapa nchini kuanzia Jumamosi tarehe 21.

Rais huyo akiandamana na mke wake Ana Dias Lourenço, waliwasili hapa nchini siku ya Alhamisi, kabla ya kuandaliwa ya siku kuu ya Mashujaa.

Alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta, Rais huyo alilakiwa na waziri wa mambo ya nje Musalia Mudavadi.

Hata hivyo, licha ya Rais huyo kuwa hapa nchini, hakuhudhuria sherehe za Mashujaa zilizoandaliwa katika uwanja wa Kericho Green, kaunti ya Kericho.

“Naomba radhi kwa niaba ya Rais wa Angola. Angependa kuwa hapa, lakini kutokana na sababu zisizoepukika, hakudhuria sherehe hizi Kericho lakini ametuma salamu za heri njema,”alisema balozi wa Angola hapa nchini António Tete.

Rais William Ruto alithibitisha kuwa, Rais huyo wa Angola yuko hapa nchini na ataanza ziara rasmi siku ya Jumamosi.

“Ataanza ziara rasmi kuanzia kesho (Jumamosi),”alisema Rais Ruto katika hotuba yake wakati wa maadhisho ya sherehe za Mashujaa katika kaunti ya Kericho.

Share This Article