Rais wa AfDB Akinwumi Adesina atunukiwa tuzo ya CGH

Martin Mwanje
1 Min Read
Rais William Ruto (kulia) akiwa na Rais wa AfDB, Dkt. Akinwumi Adesina

Rais William Ruto amemtunuku Rais wa Kundi la Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina tuzo ya Daraja la Kwanza ya Chief of the Order of the Golden Heart (C.G.H.).

Rais Ruto alimkabidhi Dkt. Adesina tuzo hiyo katika Ikulu ya Nairobi leo Jumatatu.

“Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imekuwa mstari wa mbele katika ukuaji endelevu wetu wa kiuchumi,” aliungama Rais Ruto wakati wa hafla hiyo.

“Benki hiyo siyo tu kwamba imeharakisha upatikanaji wa umeme kwa wote, imeimarisha upatikanaji wa chakula na kuhamasisha maendeleo ya miundombinu, bali pia imeimarisha utangamano wa kikanda.”

Rais Ruto alipongeza uongozi wenye ujasiri na maono wa AfDB hasa Dkt. Adesina kwa kuiwezesha Kenya  na bara la Afrika  kwa jumla kuendelea kiuchumi na kuboresha maisha ya raia wake.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *