Rais wa Marekani, Donald Trump, amesitisha mara moja msaada wa kijeshi kwa Ukraine chini ya wiki moja baada ya kufarakana na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy, katika Ikulu ya White House.
Trump anamshutumu Zelenskiy kwa kutokuwa na shukran kwa Marekani licha ya kusimama na nchi yake tangu kuzuka kwa vita baina ya Ukarine na Urusi.
Serikali ya Trump imerithi deni la dola bilioni 3.85, kutoka kwa mtangulizi wake Joe Biden zilizotengewa kuifadhili Ukraine kupitia kwa kununua zana za kivita.
Agizo hilo la Trump lina maanisha kuwa hakuna msaada mpya wa kijeshi utakaotolewa na serikali ya Marekani kwa Ukariane.
Trump na Zelenskiy walikosa kuelewana kuhusu njia ya kuleta amani nchini Ukraine walipokutana Ijumaa iliyopita.