Rais Ruto: Serikali kuboresha makao maeneo ya mijini

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto amekariri kujitolea kwa serikali yake kuboresha makao katika maeneo ya mijini kote nchini.

Amesemo hatua hiyo inalenga kuhakikisha wakazi wanaishi kwa nyumba bora kupitia kwa mradi wa ujenzi wa nyumba za bei ya gharama nafuu.

Ruto amesema haya leo Jumapili alipoongoza taifa kwenye maadhimisho ya 61 ya sherehe za Sikukuu ya Mashujaa katika kaunti ya Kwale.

Ruto amesifia ujenzi wa nyumba za gharama nafuu akiutaja kuwa muhimili mkuu wa serikali yake.

Amesema mpango huo umeendelea kutoa nafasi za ajira nchini huku ukihakikisha asilimia 60 ya Wakenya wakatakaohamia maeneo ya miji wanaishi katika makazi bora.

 

Share This Article