Rais Ruto: Waliofadhili na kupanga ghasia nchini watachukuliwa hatua

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto.

Rais William Ruto ametaja ghasia zilizoshuhudiwa leo Jumanne kote nchini, kuwa uhaini huku akiahidi kurejesha  hali ya kawaida.

Akihutubia taifa kutoka Ikulu ya Nairobi Jumanne usiku, kiongozi huyo wa taifa alitaja ghasia hizo kuwa uvamizi dhid ya demokrasia ya taifa hili, mfumo wa sheria, maadili na taasisi za kikatiba.

“Mashambulizi ya leo yamesababisha kupotea kwa maisha, uharibifu wa mali na unajisi wa taasisi na nembo zetu,” alisema Rais Ruto.

Aidha, kiongozi huyo nchi alidai kuwa ghasia hizo zilipangwa na kufadhiliwa na watu ambao hakuwataja, kwa lengo la kuyumbisha nchi hii.

Aliwahakikishia wakenya kwamba serikali itatumia rasilimali zote kuzuia kuzuka kwa tukio sawia na hilo.

“Wakenya wanapoelekea kulala, nawahakikishia usalama wenu, familia na mali yenu,” alisema Rais Tuto.

Aliwapongeza maafisa wa usalama kwa kulinda taifa hili, huku akiagiza asasi zote za usalama kuweka mikakati ya kukabiliana na ukosefu wa usalama.

Aliwaonya wale wanaofadhili ghasia kuwa serikali itachukua hatua madhubuti dhidi yao.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *