Rais Ruto: Serikali itawasaidia Wakenya wanaoishi ughaibuni

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto katika mkutano wa UNGA, Marekani.

Rais William Ruto amesema Serikali yake imejitolea kutekeleza hatua madhubuti za kuwasaidia Wakenya wanaoishi ughaibuni.

Rais alibainisha kuwa chini ya mpango mpya wa uhamaji wa wafanyakazi, serikali pia inalenga kuongeza nafasi kwa Wakenya kufanya kazi katika mataifa ya kigeni.

Rais aliyasema haya alipokutana na Wakenya wanoishi ughaibuni na kufanya  kazi katika Umoja wa Mataifa katika Ubalozi wa Kudumu wa Kenya mjini New York nchini Marekani.

Rais alijivunia kuwa zaidi ya Wakenya 1,800 wanafanya kazi katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York.

Wakati huo huo, Rais Ruto amesema kuwa Kenya inatafuta  njia za kukuza uhusiano wake na Iraq ambayo imeahidi kuwa mshirika thabiti katika biashara, kilimo na uhamaji wa wafanyakazi.

Amesema lengo kuu ni Kenya kupata soko la majani chai, kahawa na nyama ya ng’ombe katika taifa hilo la Kiarabu.

Rais alizungumza alipokutana na Waziri Mkuu wa Iraq Mohammed Shia’ Al Sudani mjini New York.

Pia walijadili kuhusu kufunguliwa kwa Ubalozi wa Kenya nchini Iraq ili kuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

TAGGED:
Share This Article