Rais Ruto: Serikali itaimarisha uhusiano wa Kenya na mataifa mengine

Tom Mathinji
1 Min Read

Rais William Ruto amesema kuwa uhusiano thabiti baina ya Kenya na nchi nyingine ni muhimu kwa ajenda ya maendeleo ya nchi hii.

Aliongeza kusema kuwa serikali itaimarisha uhusiano na mataifa mbalimbali ili kufungua fursa ambazo bado hazijatumika na kuimarisha maazimio ya biashara na uwekezaji.

Akizungumza katika ikulu ya Nairobi alipopokea hati za mabalozi na makamishna 11 wakuu, rais alisema kuwa uhusiano thabiti huiwezesha nchi hii kupata masoko mapya, kuimarisha biashara na kuanzisha mahusiano mapya baina ya Kenya na nchi nyingine.

Alisema kuwa uhusiano huo hufanikisha uhsirikiano na mataifa mengine ambao huleta fursa za ustawi wa kiuchumi na kijamii.

Mabalozi na makamishna hao 11 wakuu ni pamoja na wale kutoka Pakistan, Qatar, Tanzania, miongoni mwa nchi nyingine.

Wajumbe hao walikariri azma yao ya kujenga uhusiano thabiti na Kenya kwa manufaa ya nchi zote husika.

Sekta kuu za uhusiano walizozungmzia ni biashara, uwekezaji, uchumi wa rasilmali za majini na mabadiliko ya kidijitali, miongoni mwa nyingine.

TAGGED:
Share This Article