Rais Ruto: NYS itatumika kuimarisha uchumi wa taifa

Tom Mathinji
2 Min Read

Rais William Ruto amesema huduma ya taifa ya vijana NYS, itatekeleza wajibu muhimu katika ajenda ya serikali ya kuimarisha uchumi wa taifa hili.

Akizungumza wakati wa sherehe ya 87 ya kufuzu kwa mahafali 10,521 wa huduma ya taifa ya  vijana mjini Gilgil kaunti ya Nakuru siku ya Ijumaa, Rais alisema utawala wake utawekeza katika kuwawezesha vijana kwa maendeleo ya taifa.

Alisema serikali imewekwa mikakati mwafaka ya ya kuwapa vijana ujuzi na uwezo ili kuwafaya kuwa wenye ushindani sio tu hapa nchini lakini pia katika soko la Kimataifa.

Mahafala 10,521 wa NYS waliofuzu Ijumaa.

Kiongozi wa taifa alisema serikali imechukua ya kuwezesha taasisi za NYS kuongeza idadi ya vijana 100,000 kila mwaka katika muda wa miaka mitano ijayo.

” Mwaka huu vijana 10,000 wamefuzu. Mwaka ujao awamu ya kwanza itakuwa na vijana 15,000. Katika awamu ya pili mwezi Agosti l, vijana 15,000 watafuzu, hii ikimaamisha kuwa mwaka ujao vijana 30,000 watafuzu kutoka NYS,” alitanga kiongozi wa nchi.

Rais Ruto aliongeza kuwa baraza la usalama wa taifa tayari limeidhinisha mpango wa utakaosababisha asilimia 80 ya mahafali wa NYS kujiunga na huduma ya taifa ya polisi, vikosi vya ulinzi KDF, shirika la huduma kwa wanyamapori KWS na huduma ya taifa ya misitu KFS.

Mahafala hao walijumuisha wanaume 6,861 na wanawake 3,660 huku watu wenye ulemavu wakiwa 47.

 

Share This Article