Rais William Ruto na Mkewe, Mama Rachel Ruto wamewatakia Wakenya Sikukuu njema ya Krismasi na Mwaka Mpya wa 2025 wenye mafanikio tele.
Katika ujumbe wao, Rais na Mkewe hasa wamewapongeza wahudumu wa afya na walimu kutokana na mchango wao madhubuti katika ujenzi wa taifa.
Aidha, wamewataka Wakenya kuwa mstari wa mbele katika kupanda miti ili kusaidia katika juhudi za serikali za kutunza mazingira.
Ili kupata ufahamu wa alichokisema Rais Ruto na Mkewe katika ujumbe wao wa Sikukuu ya Krismasi kwa Wakenya, tafadhali tazama video ifuatayo: