Rais Ruto: Maamuzi yetu yataongozwa na data

Martin Mwanje
2 Min Read
Rais William Ruto wakati wa uapishaji wa Noordin Haji kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa NIS katika Ikulu ya Rais, Nairobi.

Rais William Ruto amesema serikali itatumia tathmini ya ujasusi kukabiliana na changamoto zinazochipuka duniani.

Rais Ruto amesema utumiaji wa habari inayoongozwa na data utasaidia kukabiliana na masuala sugu na magumu yanayoikabili nchi.

Rais William Ruto amesema serikali itatumia tathmini ya ujasusi kukabiliana na changamoto zinazochipuka duniani.

Rais Ruto amesema utumiaji wa habari inayoongozwa na data utasaidia kukabiliana na masuala sugu na magumu yanayoikabili nchi.

Alitaja ugaidi, ukosefu wa usalama, changamoto za kiuchumi na mabadiliko ya tabia nchi kuwa baadhi ya changamoto zinazoikabili dunia.

Alitoa wito kwa taasisi husika kuwapa wafanya maamuzi na wabunge habari za kuaminika ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao.

“Maamuzi bora yanafanywa ikiwa una habari za kuaminika,” Rais Ruto alisema.

Alielezea kuwa sera zote za serikali, sheria na hatua zingine zitajikita kwa tathmini zilizothibitishwa na uelewa.

Rais aliyasema hayo leo Jumatano wakati wa uapishaji wa Mkurugenzi Mkuu mpya Shirika la Kitaifa la Ujasusi, NIS Noordin Haji uliofanyika katika Ikulu ya Rais jijini Nairobi.

Alielezea imani yake katika uwezo na tajiriba ya Haji kuongoza NIS na kuongeza kuwa ana dhamira ya kuimarisha asasi za kikatiba ili kutoa huduma bora kwa Wakenya.

Naibu Rais Rigathi Gachagua, Waziri Mwenye Mamlaka Zaidi Musalia Mudavadi na Waziri wa Usalama wa Taifa Prof. Kithure Kindiki ni miongoni mwa waliokuwapo wakati wa hafla hiyo.

 

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *