Rais Ruto kuongoza sherehe za 88 za kufuzu kwa makurutu wa NYS

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto ataongoza sherehe za 88 za kufuzu kwa makurutu wa vijjana wa huduma kwa taifa (NYS) katika chuo cha Gilgil.

Halfa hiyo inatarajiwa kuanza mida ya saa nne asubuhi.

Siku ya Ijumaa, Naibu Kamanda wa NYS Jamlick Chabari aliongoza mwigo na matayarisho ya kufuzu kwa makurutu hao katika chuo cha Gilgil, na kuthibitisha kuwa makurutu hao wako tayari kwa hafla ya leo.

Makurutu hao wanafuzu baada ya kupokea mafunzo ya miezi sita kwa taaluma mbalimbali na pia mafunzo maalum ya kutoa ulinzi.

Ruto anatarajiwa kuandamana na Waziri wa Utumishi wa Umma Justin Muturi.

Akiongoza sherehe za kufuzu mwaka 2023, Rais alitangaza kuongeza idadi ya vijana wanaojiunga na NYS kwa nafasi 10,000, na pia kuwatengea asilimia 30 ya nafasi za ajira katika idara ya utumishi wa umma.

Hafla hiyo itapeperushwa mubashara katika runinga ya taifa ya KBC Channel 1.

Share This Article