Rais William Ruto anatarajiwa kuhudhuria tamasha ya kwanza kabisa ya jamii ya Maa inayoendelea katika mbuga ya wanyamapori ya Maasai Mara.
Tamasha hiyo ambayo ilianza rasmi jana ni jukwaa la watu wa jamii ya Maa kutoka ndani na nje ya Kenya kunadi tamaduni zao.
Inahusisha watu wa jamii hiyo kutoka kaunti za Narok, Kajiado, Samburu, Isiolo, Marsabit na kutoka nchi jirani.
Viongozi wa jamii hiyo wakiwemo magavana Joseph Ole Lenku wa Kajiado na Patrick Ole Ntutu walihudhuria siku ya kwanza ya tamasha hiyo huku wakimkaribisha Rais Ruto kwa ufunguzi rasmi.