Rais Ruto kuhudhuria mkutano wa UNGA nchini Marekani

Mkutano wa 81 wa UNGA utaandaliwa kati ya Septemba 18 na Septemba 22, Jijini New York Marekani.

Tom Mathinji
1 Min Read
William Ruto - Rais wa Kenya.

Rais William Ruto anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA), utakaoandaliwa Jijini New York Marekani.

Katibu katika wizara ya Mambo ya Nje Korir Sing’Oei, amesema kiongozi wa taifa atashiriki mkutano huo ambao utapigia kurunzi mageuzi ya kimataifa, deni la mataifa husika, ufadhili wa hali ya anga, biasahara  na usalama wa kikanda yataangaziwa pakubwa.

Kwenye mkutano na wanahabari siku ya Alhamisi, Sing’Oei alidokeza kuwa uwakilishi wa Kenya kwenye mkutano huo ni muhimu, huku ikitumia mkutano huo kuendeleza maslahi yake kwenye masuala yanayofungamana na deni la taifa, ufadhili wa tabianchi, biashara ya kidijitali na usalama wa kikanda.

Sing’Oei alisema Rais Ruto anatarajiwa kushiriki kwenye mjadala utakaoangazia athari za mabadiliko ya tabianchi, Kenya ikiwa na uzoefu baaada ya kuandaa kongamano la kwanza kuhusu tabianchi  barani Afrika.

Mkutano wa 81 wa UNGA utaandaliwa kati ya Septemba 18 na Septemba 22, Jijini New York Marekani.

Share This Article