Rais Ruto kuhudhuria mkutano wa IGAD nchini Djibouti

Tom Mathinji
1 Min Read

Rais William Ruto siku ya Jumamosi atasafiri kuelekea nchini Djibouti, kuhudhuria mkutano wa 41 wa viongozi wa serikali wa shirika la IGAD.

Marais kutoka Eritrea, Ethiopia, Somalia, South Sudan, Sudan, Uganda na wenyeji Djibouti watahudhuria mkutano huo.

Mkutano huo wa IGAD unatarajiwa kujadili maswala muhimu yanayohusu kanda hii, ambayo ni pamoja na usalama, nishati, miundomsingi na mabadiliko ya hali ya hewa.

Viongozi hao wa IGAD walielezea wasi wasi wao kuhusiana na kudorora kwa hali ya usalama nchini Sudan, huku vita kati jeshi la Sudan na wapiganaji wa Rapid Support Forces (RSF) vikizidi katika sehemu kadhaa za Khartoum na Merowe.

Share This Article