Rais Ruto kufanya ziara ya siku mbili Ujerumani

Tom Mathinji
1 Min Read

Rais William Ruto ataondoka hapa nchini Alhamisi jioni, kuelekea nchini Ujerumani kwa ziara rasmi ya siku mbili.

Ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, kitamaduni na kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.

Kulingana na msemaji wa Ikulu  Hussein Mohamed, Rais Ruto atashiriki mikutano muhimu ikiwa ni pamoja na kutiwa Saini kwa makubalino kati ya Kenya na Ujerumani kuhusu uhamiaji na uchukuzu na pia atahudhuria tamasha la Bürgerfest.

“Rais atahudhuria na kuhutubia tamasha muhimu la  “Pamoja – Stronger Together.” Kenya inakuwa taifa la kwanza lisilo la bara Ulaya ambalo limechaguliwa kushirikiana na Ujerumani katika tamasha hilo,” alisema Hussein.

Rais Ruto pia atashiriki mazungumzo na Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier na Chansela Olaf Scholz.

Kiongozi wa taifa pia atatafuta nafasi za ajira kwa vijana pamoja na fursa za elimu ya juu.

Share This Article