Rais Ruto: Kenya na Ufaransa zinapanua ushirikiano katika sekta muhimu

Tom Mathinji
1 Min Read

Rais William Ruto amesema Kenya na Ufaransa zinaendelea kufurahia uhusiano ulioimarika, huku Ufaransa ikiwa mwekezaji Mkuu hapa nchini.

Kiongozi huyo wa taifa alidokeza kuwa Mataifa hayo mawili yanapanua ushirikiano wao katika sekta muhimu ikiwa ni pamoja na ustawi wa viwanda, uchumi wa baharini, Kilimo, uchumi wa dijitali, afya na elimu, ili kubuni fursa zaidi kwa raia wake.

Akizungumza alipokutana na balozi wa Ufaransa hapa nchini Arnaud Suquet katika Ikulu ya Nairobi, Rais Ruto alidokeza kuwa wawili hao walijadili kuhusu kongamano la Africa Forward ambalo litaandaliwa Jijini Nairobi kati ya Mei 11 na 12,2026,  hili likiwa kongamano la kwanza la aina hiyo kuandaliwa katika taifa lisilozungumza Kifaransa.

“kwenye Kongamano hilo, tutaangazia maswala muhimu, ikiwa ni pamoja na kufanyia mabadiliko mfumo wa ufadhili wa kimataifa pamoja na kuimarisha ushirikiano endelevu wa kiuchumi,” alisema Rais Ruto.

Aidha viongozi hao wawili walijadili kuhusu kongamano la G7, Summit,ambapo Kenya imealikwa na Rais Emmanuel Macron.

Share This Article