Rais Ruto: Kenya na Korea Kusini kuimarisha uhusiano wa kibiashara

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais Ruto akutana na mjumbe maalum wa Korea Kusini Hong Kyum Kim.

Rais William Ruto amesema Kenya imejitolea kuimarisha uhusiano wa kibiashara baina yake na Korea Kusini.

Akiongea katika ikulu ya Nairobi alimpomlaki mjumbe maalum wa rais kutoka nchini Korea Kusini,  pamoja na naibu waziri wa kwanza wa mashauri ya nchi za kigeni, Hong Kyum Kim, Rais alisema ushirikiano huo wa kibiashara utaimarisha biashara na uchumi katika mataifa hayo mawili.

Kiongozi wa taifa alisema Kenya inadhamini ushirikiano katika ustawishaji wa taasisi za kiufundi na mafunzo TVET hapa nchini, sekta za afya ya umma, maji, usafi pamoja na teknolojia ya habari na mawasiliano baina ya mataifa haya mawili.

Alisema anatazamia kuboresha ushirikiano wa mataifa haya mawili katika kongamano lijalo baina ya Korea na mataifa ya bara Afrika.

Rais Ruto alisema mataifa haya mawili yamekubaliana kutumia nafasi zao kukuza uzingatiaji wa sheria za kimataifa na kuhimiza amani na uthabiti kote duniani.

Share This Article