Rais Ruto azuru uwanja wa Talanta Sports City

Alitoa hakikisho la kukamilishwa kwa ujenzi wa uga huo tayari kuandaa fainali za Kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2027.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto ameelezea kuridhishwa kwake na ujenzi unaoendelea wa uwanja wa Talanta Sports City katika kaunti ya Nairobi.

Rais amesema hayo alipokagua ujenzi wa uwanja huo leo Ijumaa.

Aliongeza kuwa serikali imewaajiri wafanyakazi 3,300 kwa ujenzi wa uwanja huo, 2,000 wakifanya kazi mchana na wengine 1,300, wakifanya kazi usiku.

Ruto amesema kuwa ujenzi wa viwanja na miundombinu kote nchini umewaajiri watu wapatao 250,000 kufikia sasa kote nchini kwa ajili ya ujenzi wa masoko na viwanja.

Alitoa hakikisho la kukamilishwa kwa ujenzi wa uga huo tayari kuandaa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2027.

Ujenzi wa Talanta Sports City umeratibiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Februari mwaka ujao.

Website |  + posts
Share This Article