Rais Ruto azungumza na Antonio Guterres, Hassan Sheikh Mohamud kwa njia ya simu

Tom Mathinji
2 Min Read
Rais Ruto

Rais William Ruto, Alhamisi jioni alizungumza kwa njia ya simu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  António Guterres, mazungumzo yao yakiangazia juhudi zinazoendelea za kuleta amani nchini Haiti.

Kupitia ukurasa wa X, Ruto alisema Guterres alipongeza juhudu zinazoongozwa na Kenya za kuleta udhabiti katika taifa hilo la Carebbean linalokumbwa na migogoro kutoka kwa magenge na msukosuko wa kisiasa.

Wakati huo huo, kiongozi wa taifa alimfahamisha Katibu huyo Mkuu kuhusu juhudi za amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), zinazotekelezwa kwa pamoja na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na ile ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

“Nilimjulisha kuhusu matokeo ya kongamano la pamoja la EAC na SADC, lililoendeleza jitihada za hapo awali na lililozindua mfumo mpya unaojumuisha hatua za sasa, za muda mfupi na zile za muda mrefu,” alisema Rais Ruto.

Rais alitoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuunga mkono juhudi za EAC na SADC za kuhakikisha amani inapatikana Mashariki mwa DRC.

Baadaye Rais Ruto alizungumza kwa njia ya simu na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, ambapo viongozi hao wawili walikubaliana kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi.

“Nilizungumza na Rais wa Somalia kwa njia ya simu, ambapo tulikubaliana kudumisha amani na udhabiti katika kanda hii kwa manufaa ya nchi hizi mbili,” alisema Rais Ruto kwa njia ya simu.

Wawili hao walielezea umuhimu wa juhudi za pamoja katika kushughulikia changamoto zinakomabili nchi hizo zikiwa ni pamoja na ugaidi.

Website |  + posts
Share This Article