Rais Ruto azindua ujenzi wa uga wa Talanta utakaoselehi mashabiki 60,000

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto mapema leo Ijumaa amezindua ujenzi wa uwanja wa michezo wa Talanta Sports City katika eneo la Jamhuri utakaomudu mashabiki 60,000.

Uchanjaa huo unatarajiwa kukamilika Disemba mwaka 2025 na utajumuisha uwanja wa soka, uwanja wa raga na zulia ya riadha.

Akihutubu kwenye hafla hiyo, Ruto amesema kuwa serikali itawekeza zaidi katika michezo na kuhakikisha fainali za mwaka 2027 za AFCON zitakazoandaliwa kwa pamoja na Uganda,Tanzania na Kenya zinafana.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Waziri wa Michezo Ababu Namwamba.

Share This Article