Rais William Ruto ametuma ujumbe wa heri njema ya Sikukuu ya Pasaka kwa Wakenya wote, akiwahimiza kuwa na matumaini na umoja.
Amesema kuwa Sikukuu ya Pasaka ni ishara ya mwanzo mpya kwa vitu vingi maishani.
Wakristo duniani kote hii leo, Aprili 3, wanaadhimisha Ijumaa Njema ikiwa ni kumbukumbu kwa kusulubiwa kwa Yesu Kristo msalabani kwa ajili ya dhambi za wanadamu.
Hata hivyo, kusulubiwa huko kulishindwa kabisa kufuatia kufufuka kwa Yesu Kristo siku tatu baadaye ambayo ni siku ya Jumapili.
Ikizingatiwa kufufuka huko kulifanyika siku ya Jumapili, humu nchini, siku ya Jumatatu itakuwa sikukuu ambapo Wakenya wataendelea kusherehekea ushindi uliopatikana msalabani.