Rais william Ruto ambaye amerejea nchini kutoka Ethiopia alilokuwa anahudhuria mkutano wa 37 wa viongozi wa nchi za umoja wa Afrika, tayari amefika Naivasha kwa mkutano wa baraza la mawaziri.
Mkutano huo wa pili wa kila mwaka unahusisha pia viongozi waliochaguliwa kupitia vyama tanzu vya muungano unaotawaka wa Kenya Kwanza.
Ulianza jana Februari 18, 2024 na utaendelea hadi Jumatano Februari 21, 2024 katika hoteli ya Lake Naivasha Resort.
Kulingana na hatibu wa serikali Isaac Mwaura, mkutano huo ni wa kutathmini utendakazi wa serikali katika mwaka 2023 huku ukitumiwa kuweka mikakati ya utendakazi wa serikali mwaka 2024.
Leo Jumatatu ni zamu ya wabunge wa Kenya Kwanza kupiga msasa kazi yao ya mwaka jana huku mawaziri, makatibu wa wizara na viongozi wengine wakuu serikalini wakifanya hivyo Jumanne na Jumatano.