Rais Ruto awasili Italia kuhudhuria mkutano wa G7

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto amewasili nchini Italia kwa mkutano wa G7.

Rais William Ruto amewasili Jijini Apulia nchini Italia, kuhudhuria mkutano wa mataifa saba yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi G7, ambako anatarajiwa kuhutubia mkutano huo.

Katika hotuba yake, Rais Ruto ataelezea umuhimu wa kuhusisha mataifa ya Afrika katika kutatua changamoto zinazokumba ulimwengu, kama vile mabadiliko ya tabia nchi, amani na usalama, vita na migogoro inayoshuhudiwa.

Kiongozi huyo wa taifa pia ataangazia uwezo wa Afrika katika  utumizi wa kawi safi katika viwanda, uvumbuzi na ukuaji wa dijitali.

Rais Ruto pia ataelezea mabadiliko katika Umoja wa Afrika, yanayolenga kuimarisha biashara na maendeleo, usalama na udhabiti na ushiriki wa kimataifa.

Mataifa wanachama wa G7 ni pamoja na Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, uingereza, Marekani na Muungano wa Ulaya.

Marais wengine wa Afrika wanaohudhuria mkutano huo ni Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune, Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi na Rais wa Tunisia Kais Saied.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *