Rais Ruto awaongoza Wakenya kuadhimisha siku ya Mazingira

Serikali inalenga kupanda miti bilioni 15 kufikia mwaka 2032, ikinuia kuongeza utandu wa miti nchini Kenya kwa asilimia 30.

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais Ruto awaongoza Wakenya kuadhimisha siku ya Mazingira.

Rais William Ruto leo Jumamosi ameongoza taifa kuadhimisha siku ya Mazingira ya mwaka huu katika kaunti ya Trans Nzoia.

Serikali inalenga kupanda miti bilioni 15 kufikia mwaka 2032, ikinuia kuongeza utandu wa miti nchini Kenya kwa asilimia 30.

Wiki ya Mazingira mwaka huu ilianza Oktoba 5, serikali ikijizatiti kupanda miti miti milioni 17.24 kufika mwisho wa mwezi Oktoba.

Kiongozi wa taifa aliwahimiza Wakenya kukumbatia lengo la taifa hili la kupanda miti bilioni 15 kufikia mwka 2032, ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

“Nawashukuru Wakenya kwa kushiriki katika zoezi la leo la upanzi wa miti kuunga mkono juhudi za kupanda miti milioni 5.3 kuadhimisha siku ya Mazingira,” alisema Rais Ruto.

Wakati huo huo, Rais alisambaza mbegu za mmea wa kakao (Cocoa) kwa wakulima wa Endebess, kuashiria mwanzo wa ukuzaji wa zao hilo nchini Kenya.

“Lengo letu ni kupanda miti inayolinda mazingra huku ikiwaletea wakulima mapato,” aliongeza Rais Ruto.

Rais Ruto alisema kilimo cha kakao, kitafanikisha utayarishaji bidhaa mbali mbali, wakati huo huo kikichangia kurejeshwa utandu wa miti hapa nchini.

Share This Article