Rais William Ruto, ametoa wito kwa viongozi wa Bara Afrika, kuhudhuria mkutano ujao wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabia nchi, wakiwa na sauti moja.
Rais alisema ajenda ya Afrika katika mkutano wa COP29 Jijini Baku, Azerbaijan, unapaswa kushinikiza mfumo mpya na ulio sawa wa ufadhili wa mipango ya mabadiliko ya tabia nchi, akidokeza kuwa mfumo huo unapaswa kushughulikia maswala yanayoathiri Afrika na mataifa yanayoendelea.
Rais aliyasema hayo Leo Jumatano wakati wa mkutano wa Kamati wa Marais na viongozi wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi (CAHOSCC), pembezoni mwa mkutano wa baraza la Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani.
Rais Ruto indiye mwenyekiti wa mkutano huo wa CAHOSCC.
“Leo tunawiainisha nafasi yetu kwa mkutano wa oday, wa COP29 Jijini Baku, Azerbaijan, mwezi Novemba mwaka huu,” alisema Rais Ruto.
Waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na mwenyekiti wa Tume ya Afrika Moussa Faki Mahamat na Rais wa Mauritania Mohamed Ould Ghazouani ambaye pia ni mwenyekiti wa Muungano wa Afrika.
Rais alisema uwekezaji bora barani Afrika uwe ni katika kawi safi, kilimo, au uchukuzi, ni muhimu kuhakikisha utekelezaji wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi.