Ruto atia saini kuwa sheria mswada wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu

Tom Mathinji
1 Min Read

Rais William Ruto leo Jumanne katika ikulu ya Nairobi ametia saini kuwa sheria mswada wa ujenzi wa nyumba za gharama  nafuu.

Hatua hiyo inajiri siku chache baada ya bunge la taifa kupitisha mswada huo.

Rais Ruto alisema punde tu baada ya kutia saini mswada huo kuwa sheria, Wakenya watatozwa ushuru wa nyumba za gharama nafuu wa asilimia 1.5 huku mwajiri naye akilipa asilimia 1.5.

Kiongozi wa taifa alisema mpango wa ujenzi wa nyumba hizo za gharama nafuu utatoa nafasi za ajira kwa vijana nchini pamoja na kuhakikisha kuna ardhi ya kutosha kwa kilimo.

Mnamo mwezi Novemba mwaka 2023, mpango huo wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu ulipata pigo, baada ya Mahakama Kuu kusema ushuru wa mradi huo unaotozwa Wakenya ni kinyume cha katiba.

Website |  + posts
Share This Article