Rais Ruto ateua wenyeviti na wanachama wa tume na bodi mbalimbali

Marion Bosire
2 Min Read
Rais William Ruto

Rais William Ruto ameteua wenyeviti na wanachama wa bodi na tume mbalimbali humu nchini.

Katika taarifa iliyotiwa saini na mkuu wa utumishi wa umma Felix Koskei, Rais aliteua wenyeviti na wanachama wa bodi ya mamlaka huru ya kutathmini utendakazi wa polisi IPOA na tume ya utekelezaji haki CAJ.

Aliteua pia wa tume ya mishahara na marupurupu SRC pamoja na wa tume ya usawa wa kijinsia nchini NGEC.

Aliyekuwa mwenyekiti wa IEBC Ahmed Issack Hassan amependekezwa kuwa mwenyekiti wa bodi ya IPOA huku Ann Wanjku Mwangi, Micah Onyiego Nyakego, Boniface Kipkemoi Samati, Annette Mbogoh, John Muchiri Nyaga, Kenwilliams Nyakomitah na Jackline Lukalo Mwenesi wakipendekezwa kuwa wanachama wa bodi hiyo.

Charles Orinda Dulo amependekezwa kuwa mwenyekiti wa tume ya utekelezaji haki CAJ na wanachama waliopendekezwa ni Charles Njagua Kanyi na Dorothy Jemator Kimengech.

Katika tume ya mishahara na marupurupu Rais amependekeza Sammy Chepkwony kuwa mwenyekiti huku Martin Kizito Ong’oyi, Mohamed Aden Abdi, Jane Gatakaa Njage, Leonid Ashindu, Gilda Odera na Geoffrey Apollo Omondi wakipendekezwa kuwa wanachama.

Rehema Dida Jaldesa amependekezwa kuwa mwenyekiti wa tume ya usawa wa jinsia huku Michael Mbithuka Nzomo akiteuliwa mwanachama.

Rais amemteua pia Gerald Nyaoma Arita kuwa naibu gavana wa pili wa benki kuu ya Kenya.

Kiongozi wa nchi alifafanua kwamba aliafikia uteuzi huo kufuatia mapendekezo kutoka kwa kamati za uteuzi.

Website |  + posts
Share This Article