Rais William Ruto kwa mara ya kwanza amejitokeza kimasomaso kutetea mpango wa uwekezaji wa kampuni ya Adani kutoka India kwenye kampuni ya KETRACO.
Ruto aliyekuwa akizungumza kwenye kiwanda cha kuzaliza umeme wa mvuke cha Menengai Ruto amesema mkataba huo wa shilingi bilioni 95, utasaidia kupunguza gharama ya umeme.
Rais amesisitiza kuwa Adani watajenga laini kadhaa mpya za kusambaza umeme, hatua itakayomaliza tatizo la upungufu wa nguvu za umeme wa mara kwa mara nchini.
Adani watasimamia na kuendesha KETRACO kwa kipindi cha miaka 30 ijayo.