Rais Ruto atetea hatua yake ya kubuni serikali jumuishi

Dismas Otuke
1 Min Read
Rais William Ruto.

Rais William Ruto ametetea hatua yake ya kubuni baraza la Mawaziri linalowajumuisha viongozi wa kutoka chama cha upinzani  cha  ODM,akisema alifanya hivyo makusudi ili kuboresha utoaji huduma na utendakazi.

Akiongoea kwenye kikao na wananchi katika kauntoi ya Mombasa Jumapili jioni,Ruto amesema punde tu Mawaziri hao watakapoidhinishwa, wataisaidia serikali yake kuafikia ruwaza na malengo yake.

Ameongeza kuwa sera  nyingi za  muungano wa upinzani na  zile za chama chake cha UDA zilikuwa sawia na uteuzi wa wanasiasa kutoka ODM, kamwe hakutahujumu utendakazi wa serikali yake.

Kwenye kikao hicho na umm Ruto amekariri kujitolea kwa serikali yake kubuni nafasi za ajira, ikiwemo kuongeza  ushuru kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ya nchi, ili kukuza viwanda vya humu nchini.

Share This Article