Rais Ruto kufungua rasmi mkutano wa Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi Afrika

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto.

Rais William Ruto leo Jumanne atafungua rasmi mkutano wa Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi wa mwaka huu (ACHOD25), utakaoadaliwa Jijini Nairobi.

ACHOD hutoa fursa kwa viongozi wa kijeshi Barani Afrika kukutana, kushauriana na kushughulikia changamoto za kiusalama.

Kupitia mashauriano, ubadilishanaji maarifa na ukuzaji ushirikiano, kongamano hilo linalenga kuhakikisha udhabiti na kuleta pamoja juhudi za kuimarisha usalama.

Kongamano hili la Nairobi, ndilo la pili kuandaliwa nchini Kenya.

Wakati huo huo Vikosi vya Ulinzi nchini (KDF) vitaanza sherehe za kufuzu za chuo cha taifa cha mafunzo ya ulinzi, leo Jumanne.

Waziri wa Ulinzi Soipan Tuya, ataongoza sherehe hizo katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi mtaani Karen.

Website |  + posts
Share This Article