Rais William Ruto mapema Ijumaa ameshuhudiwa kutiwa sahihi kwa mkataba wa ujenzi wa ukumbi na uwanja wa kisasa wa michezo jijini Nairobi, ujulikanao kama Nairobi Railway City Project.
Hatua hiyo itashuhudia kuwepo kwa uwanja wa kisasa na ukumbi wa michezo na burudani katikati ya jiji la Nairobi.
Mkataba huo umesainiwa baina ya kampuni ya Zaria Group itakayojenga mradi huo na shirika la reli nchini, ambalo limetoa kipande cha ardhi.
Mradi huo utakamilika katika kipindi cha mwaka mmoja ujao na kutoa nafasi za ajira taktiban 25,000 kwa kila mwaka.