Rais Ruto ashauriana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto.

Rais William Ruto amesema ameshauriana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio,ambapo waliangazia kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Kenya na Marekani.

Kupitia ukurasa wa X, kiongozi wa taifa alisema pia walijadili kuhusu amani na usalama wa kikanda, hususan mzozo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

“Tulisisitiza kuhusu jukumu muhimu linalotekelezwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa ushirikiano na Ile ya kusini mwa Afrika (SADC) katika kutuliza hali na kuleta amani. Hii inajumuisha kuwateua wapatanishi, usitishaji ghasia na kutafuta suluhu la kudumu Kupitia mchakato wa kisiasa,” alisema Rais Ruto.

Wakati huo huo Rais Ruto, alisema walijadili hali ilivyo nchini Sudan na wajibu wa Kenya wa kutoa fursa kwa wadau muhimu vikiwemo vyama vya kisiasa, mashirika ya kijamii miongoni mwa wengine, kushiriki mchakato wa kusitisha machafuko ili kutoa fursa kwa upatikanaji wa amani.

Sudan na DRC kwa sasa zinakabiliwa na ukosefu wa usalama, ambapo maelfu ya watu wamepoteza maisha, mamilioni wakitoroka makwao, huku waathiriwa wengi wakiwa wanawake, watoto na wanaoishi na ulemavu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *