Rais Ruto ashauriana na balozi wa Uingereza hapa nchini

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto na balozi wa Uingereza hapa nchini Neil Wigan

Rais William Ruto leo Ijumaa alishiriki mazungumzo na balozi wa Uingereza hapa nchini Neil Wigan, katika ikulu ndogo ya Kisumu.

Rais Ruto, ambaye kwa sasa yuko katika ziara ya maendeleo eneo la Nyanza, alielezea ushirikiano thabiti uliopo kati ya Kenya na Uingereza.

“Kenya na Uingereza zinafurahia uhusiano wa kihistoria wenye misingi ya kiuchumi, kitamaduni na baina ya raia wa nchi hizo. Uhusiano huu umenufaisha raia wa nchi hizo mbili,” alisema Rais Ruto kupitia taarifa kwa ukurasa wa X.

Akiwa katika ziara eneo la Nyanza, rais Ruto alizindua miradi kadhaa ya maendeleo katika kaunti ya Siaya.

Miongoni mwa miradi iliyozinduliwa ni pamoja na mradi wa Mageta wa kuzalisha nguvu za umeme kupitia miale ya jua, ili kupiga jeki upatikanaji wa umeme katika eneo hilo.

Share This Article