Rais Ruto asema Kenya iko makini kumaliza Ukimwi kati ya watoto kufikia 2027

Marion Bosire
1 Min Read

Rais William Ruto amesema Kenya inajitahidi kumaliza ugonjwa wa ukimwi kati ya watoto kufikia mwaka 2027.

Akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya mpango wa Rais wa Marekani wa usaidizi wa kukabiliana na ukimwi, Rais alisema kwamba ajenda hiyo ni kujitolea kwake chini ya muungano wa kimataifa.

Alisema mpango wa serikali wa huduma bora za afya kwa wote unatoa fursa ya kuziba pengo la ufadhili humu nchini unaohusiana na maradhi hayo.

“Huu ndio wakati wa kufidia muda uliopotea kwa ajili ya watoto wetu.” alisema kiongozi wa nchi.

Rais Ruto pia alisifia ushirikiano uliopo kati ya Kenya na Marekani katika vita dhidi ya ukimwi ambapo anasema mpango huo wa Rais wa Marekani wa ufadhili wa kukabiliana na ukimwi umesaidia Kenya kupiga hatua muhimu katika vita hivyo.

Hafla hiyo ya kuadhimisha miaka 20 ya mpango wa Rais wa Marekani wa ufadhili wa kukabiliana na ukimwi uliandaliwa katika maktaba ya kitaifa jijini Nairobi.

Ilihudhuriwa na balozi wa Marekani nchini Meg Whitman na waziri wa afya Susan Nakhumicha kati ya viongozi na washikadau wengine wa sekta ya afya.

Website |  + posts
Share This Article