Rais Ruto arejea kutoka Marekani

Marion Bosire
1 Min Read

Rais William Ruto amerejea nchini Kenya baada ya ziara ya kiserikali ya siku nne nchini Marekani.

Kiongozi wa nchi alilakiwa katika uwanja wa ndege na waziri wa usalama wa taifa Kithure Kindiki, mkuu wa utumishi wa umma Felix Koskei, katibu wa usalama wa ndani Raymond Omollo kati ya viongozi wengine wakuu serikalini.

Rais Ruto alisema kupitia akaunti mbali mbali za mitandao ya kijamii kwamba anafurahia kurejea nyumbani baada ya ziara hiyo iliyojiri wakati Kenya na Marekani zinaadhimisha miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia.

Wakati wa ziara hiyo rais Ruto na mweyeji wake Joe Biden waliahidi kuimarisha uhusiano kati ya mataifa haya mawili kwa manufaa ya raia wake.

Hii ndiyo ziara ya kwanza ya aina hiyo ambayo imefanywa na kiongozi wa taifa la bara Afrika katika muda wa miaka 16 iliyopita.

Share This Article