Rais William Ruto alikuwa miongoni mwa maelfu ya waombolezaji waliohudhuria mazishi ya mbunge wa Emurua Dikirr, Johana Ngeno siku ya Ijumaa katika kaunti ya Narok.
Ruto alimlimbikizia sifa marehemu Ng’eno kwa kuwa na msimamo mkali na kujitolea kwake kuhakikisha mradi wa serikali wa nyumba za gharama nafuu unafaulu.
Aidha,Rais alipendekeza kubadilishwa kwa jina la soko la Shauri Moyo na kuitwa Johana Ng’eno kama njia ya kumuenzi.
Nge’no ambaye alikuwa akihudumu muhula wa tatu bungeni alifriki baada ya Ndege waliyokuwa wakisafiria kuanguka katika kaunti ya Nandi wiki iliyopita na kuwaua abiria wote sita waliokuwamo.
Marehemu amemwacha mjane na watoto wawili wa kike.