Rais William Ruto mapema Ijumaa ameongoza mahafala ya kufuzu kwa wanajeshi katika chuo kijeshi cha Lanet kaunti ya Nakuru.
Maafisa hao wa kijeshi maarufu kama Cadets, wamefuzu kujiung na vikosi vya jeshi baada ya kuhudhuria mafunzo ya miezi sita huku wengine wakifunzwa kwa miezi minane.
Ruto amewahimiza maafisa hao kutekeleza majukumu yao kwa uwajibikaji na utaalam kuzingatia mafunzo waliyopokea chuoni.