Rais Ruto amwomboleza Rais Geingob wa Namibia

Marion Bosire
1 Min Read
Rais William Ruto.

Rais William Ruto amemwomboleza Rais Hage Geingob wa Namibia ambaye ameaga dunia hivi leo akimtaja kuwa kiongozi wa kipekee aliyetumikia watu wa Namibia kwa kujitolea.

Ruto ambaye kwa sasa anahudhuria ibada ya madhehebu mbali mbali huko Kakamega, aliendelea kumsifia akisema alikuwa na imani ya kuafikia Afrika yenye umoja na ambaye alikuwa akitetea sauti ya bara hili na kuonekana kwake katika jukwaa la kimataifa.

Kiongozi wa taifa vile vile ametoa pole zake kwa jamii ya Geingob na watu wa Namibia kwa jumla kufuatia kifo chake.

“Mwenyezi Mungu awape watu wa Namibia nguvu wakati huu mgumu.” alisema Rais Ruto kwenye taarifa.

Rais Geingob amefariki alfajiri ya leo katika hospitali ya Lady Pohamba jijini Windhoek ambapo alikuwa anapokea matibabu.

Website |  + posts
Share This Article