Rais Ruto amuomboleza mzee Isaac Ichung’wa Ngugi

Martin Mwanje
1 Min Read
Rais Wiiliam Ruto amuomboleza Mzee Isaac Ngugi, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 105.

Rais William Ruto amewaongoza viongozi nchini kuomboleza kifo cha mzee Isaac Ngugi ambaye ni babake mzazi mbunge wa Kikuyu Kimani Ichung’wah.

Kupitia ukurasa wa X, kiongozi wa taifa alimtaja marehemu mzee Ngugi kuwa mfanyabiashara mwenye bidii, hekima na mmoja wa waanzilishi wa Mji wa Kikuyu.

Rais alisema mzee Ngugi aligusa maisha ya watu wengi kupitia juhudi zake nyingi za kuleta mabadiliko ambazo zilisaidia wanyonge, akisema urithi wake utaendelea kuwasaidia.

“Mzee aligusa maisha ya wengi kupitia juhudi zake zilizoleta mabadiliko na ambazo ziliwapiga jeki wasiojiweza katika jamii,” alisema Rais Ruto.

Na katika rambirambi zake, Spika wa Bunge la Taifa Moses Wetang’ula, alisema urithi wa mzee Ngugi utadumu na kudhaminiwa na vizazi vijavyo.

Waziri wa Afya Aden Duale alitambua mchango wa Mzee Ngugi kwa jamii, akimtaja kama mtu ambaye huduma na ukarimu wake uligusa maisha ya watu wengi.

Katibu katika wizara ya usalama wa taifa Raymond Omollo pia alitoa heshima zake kwa marehemu, akiangazia jukumu la marehemu katika kuubadilisha Mji wa Kikuyu na kusaidia watu wasiojiweza.

Mzee Ngugi, ambaye alifariki akiwa Kikuyu, alikuwa na umri wa 105.

Website |  + posts
Share This Article