Rais Ruto amuaga balozi wa Congo Brazzaville anayeondoka

Tom Mathinji
1 Min Read

Rais William Ruto leo Jumanne, amemuaga balozi wa Congo Brazzaville Jean Pierre Ossey, anayeondoka hapa nchini baada ya kukamilisha kipindi chake cha kuhudumu.

Wakati wa hafla hiyo iliyoandaliwa katiku Ikulu ya Nairobi, Rais Ruto alimpongeza balozi Ossey kwa juhudi zake za kuimarisha uhusiano baina ya Kenya na Congo Brazzaville.

“Ninampongeza balozi Ossey kwa juhudi zake za kuimarisha uhusiano wa nchi hizi mbili,” alisema Rais Ruto.

Kulingana na Rais Ruto, biashara kati ya nchi hizo mbili umeimarika, huku utangamano wa raia wa mataifa hayo mawili ukiboreshwa.

“Kenya na jamuhuri ya Congo zimeimarisha uhusiano wao wa kidiplomasia na utangamano wa raia wao. Hatua hiyi imeboresha biashara na uhusiano wa kitamaduni,” alisema Rais Ruto.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *