Rais Ruto amteua Munyori Buku kuwa mkuu wa PCS

Martin Mwanje
1 Min Read
Munyori Buku - Mkuu mpya wa PCS

Munyori Buku ndiye Mkuu mpya wa Idara ya Mawasiliano ya Rais, PCS.

Awali, wadhifa huo ulishikiliwa na David Mugonyi ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano, CA.

Uteuzi wa Buku kumrithi Mugonyi kwenye wadhifa huo umetangazwa na msemaji wa Ikulu ya Nairobi Hussein Mohamed.

“Bw. Buku analeta tajiriba ya zaidi ya miaka 26 ya ngazi za juu katika mawasiliano ya kimkakati katika sekta za umma na za kibinafsi,” alisema Mohamed katika taarifa.

Kabla ya uteuzi wake, Buku alihudumu kama Katibu wa Mawasiliano ya Umma katika Ikulu ya Nairobi.

Aidha, Buku amewahi kuhudumu kama Mkurugenzi Mwandamizi wa Mawasiliano ya Umma katika Ikulu ya Nairobi, Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Wizara ya Fedha na Meneja Mhariri wa Bodi ya Uhariri ya Kenya Yearbook.

Katika sekta ya kibinafsi, Buku amewahi kuhudumu katika mashirika ya Nation Media Group na Standard Media Group.

 

Share This Article