Rais Ruto ampongeza Rais mpya wa Namibia

Tume ya Uchaguzi nchini Namibia ilitangaza matokeo rasmi ya uchaguzi ulioandaliwa wa urais, ikisema kwamba Netumbo alijizolea asilimia 57 ya kura zilizopigwa.

Marion Bosire
1 Min Read
Rais William Ruto.

Rais wa Kenya William Ruto amempongeza Netumbo Nandi-Ndaitwah baada yake kuchaguliwa kuwa Rais wa tano wa taifa la Namibia na wa kwanza wa kike.

Rais Ruto amesema kuchaguliwa kwa Netumbo ambaye ni Rais wa nne wa kike barani Afrika ni dhihirisho tosha kwamba kiongozi yeyote ana uwezo wa kuafikia cheo chochote kisiasa.

Tume ya Uchaguzi nchini Namibia ilitangaza matokeo rasmi ya uchaguzi ulioandaliwa wa urais ikisema kwamba Netumbo alijizolea asilimia 57 ya kura zilizopigwa.

Alimpiku mpizani wake wa karibu Panduleni Itula aliyejipatia asilimia 26.

Netumbo atakapoapishwa ,ataingia kwenye orodha ya Marais wa kike barani Afrika ikiwa ni pamoja na Samia Suluhu Hassan wa Tanzania.

Aidha, viongozi wengine kadhaa barani wamempongeza wakisema kuchaguliwa kwake ni dhihirisho la uthabiti wa kidemokrasia.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *