Rais Ruto alifanyia mabadiliko Baraza lake la Mawaziri

Dismas Otuke
1 Min Read
Rais William Ruto.

Rais William Ruto amefanya mabadiliko kwenye Baraza lake la Mawaziri akiwateua wandani wa mtangulizi wake Uhuru Kenyatta.

Kwenye mabadiliko hayo, aliyekuwa Waziri wa Afya Mutahi Kagwe ameteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo na Mifugo.

Gavana wa zamani wa Kiambu William Kabogo ameteuliwa kuwa Waziri  wa Habari, Mawasiliano na Uchumi Dijitali.

Gavana wa zamani wa Nakuru Lee Kinyanjui,ameteuliwa kuwa Waziri mpya wa Biashara, Uwekezaji na Viwanda.

Aliyekuwa Waziri wa Kilimo Dkt. Andrew Karanja ameteuliwa kuwa Balozi wa Kenya nchini Brazil huku mwenzake katika Wizara ya Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali Dkt. Margaret Ndung’u akiteuliwa kuwa Balozi wa Kenya nchini Ghana.

Salim Mvurya ameteuliwa kuwa Waziri wa Michezo kumrithi Kipchumba Murkomen ambaye ameteuliwa kuwa Waziri mpya wa Usalama wa Taifa.

Majina ya wote hao yamewasilishwa katika Bunge la Taifa ili kupigiwa msasa na kuidhinishwa kwa mujibu wa katiba.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *