Rais William Ruto amehudhuria mazishi ya Rais wa Namibia Hage Geingob siku ya Jumamosi mjini Windhoek Namibia.
Ruto ameahidi kushirikiana na kuisaidia serikali ya Namibia.
Rais amemtaja marehemu kuwa kiongozi shupavu na mweledi na aliyeweka mbele maslahi ya bara Afrika.
Geingob aliye na umri wa miaka 82 alifariki dunia mapema mwezi kutokana na saratani.
Marais 18 na waakilishi wengine 27 wamehudhuria mazishi hayo ya kijeshi.