Rais Ruto aanzisha WRC Safari Rally Kenya

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto ameanzisha rasmi makala ya mwaka huu ya 73, ya mashindano ya mbio za magari WRC Safari Rally nje ya jumba la Charter.

Ruto alielezea umuhimu wa mashindano hayo na fursa zinazoambatana nayo na kuwataka Wakenya kuzitumia vyema.

Rais amefichua kuwa wameanza mazungumzo na kampuni ya Toyota Gazoo, ili kutoa mafunzo kwa madereva wa humu nchini.

Jumla ya magari 39 yanashiriki mashindano hayo ya siku nne yakiwa ya mkondo wa tatu katika kalenda ya msururu wa dunia, baada ya  Monte Carlo na Uswidi.

Kati ya madereva hao 11, 10 ni wa humu nchini, wengi wakishiriki kitengo cha WRC2, WRC3 na kitengo cha kitaifa.

Baada ya kuanzishwa nje ya ukumbi wa Charter, magari hayo yameshindana katika kituo maalum cha Kasarani, kabla ya kuelekea Naivasha.

Mjini Naivsaha magari hayo yatashindana kwa siku tatu na kukamilisha jumla ya masafa ya kilomita 384.86.

Madereva tisa wanashindana katika kitengo kikuu cha WRC 1 wakiwemo watatu kutoka Toyota; Elfyn EVANS,Kalle ROVANPERÄ na Takamoto Katsuta;Thierry Neuvile wa Hyundai Shell Mobis na wenzake Martin JÄRVEOJA na Ott Tanak pamoja wale M-Sport Ford wakiwa;Josh MCERLEAN,Grégoire MUNSTER na Jourdan SERDERI.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *