Rais Ruto aanza ziara nchini Norway

Pia Ruto ameratibu ziara nyingine nchini Finland.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto ameanza ziara rasmi ya kiresikali nchini Norway, anakotarajiwa kusaini mikataba kadhaa ya ushirikiano baina ya Kenya na nchi hiyo.

Ruto aliwasili nchini Norway mapema leo Jumanne, baada ya kukamilisha ziara nyingine ya kufana nchini Ubelgiji siku ya Jumatatu.

Ruto pia ameratibu ziara nyingine nchini Finland.

Katika siku ya kwanza ya ziara yake, Rais Ruto alikutana na viongozi wa bunge la Ulaya, Baraza la Umoja wa Ulaya na pia kufanya mazungumzo na Mfalme Phillipe wa Ubelgiji.

Share This Article