Rais wa Urusi Vladimir Putin amekaribishwa rasmi nchini Korea Kaskazini baadaya kuwasili Pyongyang usiku wa manane na kulakiwa katika uwanja wa ndege na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.
Vyombo vya habari nchini humo vinaripoti kuwa viongozi hao wawili walijadili namna ya kuimarisha mahusiano na kile wanachokitaja kubadilishana mawazo.
Hii ni ziara ya kwanza ya Rais wa Urusi nchini Korea Kaskazini kwa kipindi cha miaka ishirini na tano.
Urusi inapokea silaha nzito ikiwemo makombora ya masafa marefu kutoka kwa Korea Kaskazini nayo inaipa chakula,nishati,teknolojia miongoni mwa mengine.
Putin na Kim pia watashiriki katika hafla rasmi ya kumkaribisha kiongozi huyo wa Urusi katika viwanja vya Kim Il Sung.
Hayo yatafuatiwa na mazungumzo ya kidiplomasia, pamoja na kutembelea kanisa la Orthodox miongoni mwa mambo mengine.
Pia inatarajiwa kuwa wawili hao watatia saini makubaliano mbalimbali, kuanzia uchumi hadi usalama.
Jambo kuu la mazungumzo ingawa – wataalam wanasema – litakuwa ni kujadili jinsi mataifa yaliyotengwa zaidi yanavyoweza kuimarisha uhusiano wao wa kijeshi, wakati Putin anatazamia kuongeza usambazaji wake wa silaha na silaha kwa vita vyake nchini Ukraine.